24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Pinda ashtushwa Katavi kusifika kwa ushirikina

Na Walter Mguluchuma-Katavi 

WAZIRI Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda ameonekana kushangazwa na Mkoa wa Katavi kusifika kwa imani za kishirikina, licha ya kuwa miongoni  mwa mikoa ya mwanzo kabisa kuingia kwa dini ya Romani Katoliki miaka 135 Iliyopita.

Alisema sifa hiyo ni mbaya na inatia aibu mno.

Pinda aliyasema hayo jana, wakati wa ibada ya kusimikwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Mpanda,  Eusebius Nzigilwa.

Alisema mkoa huo, pamoja  na  dini  kuingia mapema bado umeendelea  kuwa  na sifa ya kuwa na uchawi, jambo  ambalo  sasa halipo, hivyo watu wasiwe na hofu ya kuutembelea.

Alisema  ushirikina sio  sifa nzuri kabisa, unaharibu sifa ya mkoa huu ambao bado ni mpya, lakini umekuwa na maendeleo makubwa ya kiuchumi.

Alisema kanisa limekuwa na mchango mkubwa  wa kuleta maendeleo ya nchi  na limetoa mchango wa kuinua elimu  na kuboresha afya ya Wanzania  ambao wamekuwa wakipata huduma za afya kwenye vituo vyake.

Alisema Serikali inathamini michango ambayo imekuwa ikitolewa na viongozi wa dini, hivyo wanaendelea kutoa ushirikiano mkubwa kwa madhehebu yote ya dini bila kufanya ubaguzi wowote ule .

Alisema rais amefikisha taifa kwenye uchumi wa kati kuna kazi kubwa imefanyika.

Aliwataka Watanzania  wamtie moyo  Rais Dk. John Magufuli ili taifa  lizidi  kuendelea,kuna baadhi ya mataifa  yameanza kuona wivu mafanikio yanayoendelea kupatikana.

Rais wa  Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki, Askofu  Gerevansi Nyaisonga alisema kanisa hilo litaendelea kushilikiana na Serikali  kuendeleza amani ya nchi ili amani iliyopo izidi kuendelea na nchi zidi kuwa na amani zaidi .

Aliomba ushirikiano ulipo sasa na madhehebu ya diniuzidi kuendelea na wao wataendelea  kuhubiri amani.

 Askofu  Nzigilwa alisema  amekwenda Jimbo la Mpanda kuwa mtumishi na wala sio mtumikiwa.

Jimbo hilo lina  waamini 231,000 kati ya wakazi 825,880 ya wakazi wa Mkoa wa Katavi  kwa mujibu ya sensa ya mwaka jana.

Askofu Nzigilwa  aliwekwa wakfu wa  kuwa Askofu msaidisi wa Jimbo kuu la  Dares  Salaam Machi  19, 2010.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles