30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Paul Rusesabagina achungulia kifungo cha maisha jela

Kigali, Rwanda

Waendesha mashtaka nchini Rwanda wameomba kifungo cha maisha na kifungo cha miaka 170 gerezani Paul Rusesabagina anayetuhumiwa kwa mashtaka tisa ya ugaidi yanayohusiana na shambulio baya la waasi la kati ya mwaka 2018 na 2019.

Mwendesha mashtaka amesema Rusesabagina alihusika moja kwa moja kama kiongozi wa kisiasa kulingana na kauli zake, maoni yake ya sauti na kuona kwenye YouTube, na mashuhuda ya watuhumiwa wenzao.

Rusesabagina, aliyepata umaarufu kutokana na filamu ya ‘Hotel Rwanda’ ya Hollywood kuhusu mauaji ya kimbari ya Rwanda, amejiondoa katika kesi yake mwezi Machi na kusema “hatarajii kutendewa haki” katika mahakama hiyo.

Katika kesi hiyo hiyo zaidi ya washukiwa 20, upande wa mashtaka uliomba hukumu ya kifungo cha miaka 25 dhidi ya Callixte Nsabimana anayefahamika kama Sankara- msemaji wa zamani wa waasi wa FLN, ambaye alikamatwa na kurudishwa Rwanda kutoka Comoros mwaka 2019.

Mwezi Agosti mwaka jana, Rusesabagina alihadaiwa na kupandishwa ndege kutoka Dubai hadi Rwanda, hatua ambayo alitaja kuwa utekaji nyara.

Mwezi uliopita akiwa mjini Paris, Rais Paul Kagame alisema yeye mwenyewe anatarajia uamuzi wa haki katika kesi hiyo, akijibu madai ya mashataka yasiyokuwa ya haki kutoka kwa mashirika ya Marekani na Ulaya.

Mahakama kuu mjini Kigali inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo ambayo inafuatiliwa kwa karibu nchini Rwanda kwa miaka kadhaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles