32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

PAPA FRANCISCO AFUTA ADHABU YA KIFO

VATICAN CITY, VATICAN


KIONGOZI wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francisco, amesema adhabu ya kifo haikubaliki kwa hali yoyote ile na Kanisa hilo linapaswa kuanzisha kampeni ya kufuta adhabu hiyo.

Mabadiliko hayo yametangazwa juzi na kuungwa mkono na wanaharakati wanaopinga adhabu ya kifo na kuwakasirisha wakosoaji wakubwa wa kiongozi huyo, waliosema hakuwa na haki ya kubadili kile kilichoandikwa kwenye Biblia na kufundishwa kwa karne nyingi katika Kanisa Katoliki.

Kwa upande wake, Kanisa Katoliki limesema Papa Francisco amefanya mabadiliko ya mafundisho rasmi ya Kikatoliki kuonesha kwamba hukumu ya adhabu ya kifo haiwezi kamwe kutolewa, kwa sababu inakwenda kinyume cha ubinadamu.

Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International, ambalo kwa miaka mingi limekuwa likipigania kuondolewa kwa adhabu hiyo, limeyapokea mabadiliko hayo kwa mikono miwili na kusema ni hatua muhimu ya kusonga mbele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles