30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

PAPA FRANCIS ABUSU MIGUU YA KIIR NA MACHAR KUHAMASISHA AMANI SUDAN KUSINI

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amefanya tendo la unyenyekevu na ambalo halikutarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, kuwahamasisha kuuendeleza mchakato wa amani.

Mwishoni mwa ziara ya kiroho ya siku mbili ya viongozi hao wa Afrika mjini Vatican, Papa Francis alimuomba rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na hasimu wake Rieck Machar kuendeleza mazungumzo ya amani, licha ya kuongezeka kwa ugumu, na kisha alipiga magoti na kubusu miguu yao, pamoja na ya makamu wa rais Rebecca Nyendeng Garang.

Papa Fransic hufanya tendo la kitamaduni la kiimani la kuwaosha miguu wafungwa siku ya Alhamisi kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kama hili kwa viongozi wa kisiasa.

Alisema mwishoni mwa ziara hiyo kwamba anataraji kusitishwa kwa uadui, mapigano, mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles