32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘ONDOA ZIRO KISARAWE’ YAKUSANYA MIL 65/-

Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani imekusanya zaidi ya Sh milioni 65 kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa kidato cha nne waliopo kambini wakijiandaa na mitihani ya mwisho mwaka huu.

Fedha hizo zimekusanywa katika harambee iliyoongozwa na Waziri Mteule, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo amesema, katika kampeni maalumu ya ‘Ondoa Ziro Kisarawe’ yenye lengo la kusaidia kuongeza ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne wilayani humo.

“Tuwasaidie vijana wetu ambao wako kambini tangu Oktoba 30, na walimu wao wakifanya mazoezi na kujisomea na walimu wao, mpango wetu ulikuwa mtoto akikaa siku 30 za utulivu ili aweze kufanya mitihani yake vizuri, maana yake ni Sh milioni 30, naamini zitapatikana kwa mpango wa Mungu, .

“Tujipange kuondoa ziro siyo kutengeneza mimba, kama tutafeli katika hilo hakutakuwa na sababu ya kupoteza muda kuchangisha watu fedha,” amesema Jafo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Happiness Seneda, amesema wilaya hiyo ukosefu wa chakula shuleni, utoro wa wanafunzi na uhaba wa mabweni ni changamoto kubwa kwa ufaulu wa wanafunzi wa kidato cha nne wilayani humo.

“Wilaya ya Kisarawe na Mkoa wa Pwani kwa ujumla, tunaongoza kwa kuwa na viwanda vingi lakini vijana wetu hawaajiriki, tunashangaa fursa zipo hapa hapa lakini haziwasaidii vijana wetu,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Seneda amesema kampeni ya ondoa ziro imelenga kuondoa kabisa daraja hilo kwa wanafunzi wa kidato cha nne kulinganisha na takwimu za mwaka jana ambapo wanafunzi waliopata ziro walikuwa 457 huku waliopata daraja la kwanza wakiwa saba.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles