32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

 ‘OLE WENU MTAKAOSHINDWA KUWAANDIKISHA WALEMAVU SHULENI’

Na RAMADHAN HASSAN-KONGWA

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma, White Zuberi, amesema wazazi na walezi wenye watoto walemavu watachukuliwa hatua kama watawaficha watoto wao majumbani wakati wa uandikishaji wa watoto shuleni.

Zuberi alitoa onyo hilo jana, wakati alipokuwa akifungua semina ya ufuatiliaji wa mapato na matumizi ya rasilimali za umma kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Semina hiyo iliwashirikisha viongozi wa Serikali kuanzia ngazi ya vijiji hadi wilayani.

“Hapa wilayani kumekuwa na changamoto kwa upande wa wazazi na walezi wenye watoto ambao ni walemavu kwa kutoona umuhimu wa kuwaandikisha shule watoto wao.

“Kutokana na changamoto hiyo, bado kuna kundi kubwa la watoto wenye ulemavu ambao wamenyimwa fursa ya kupata elimu kwa sababu wazazi au walezi wao wanawaficha nyumbani.

“Kwa hiyo, kwa kushirikiana na jamii, tutalazimika kuwafuatilia majumbani watoto hao ili waweze kupelekwa shule na kuandikishwa na baadaye waliowaficha watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Zuberi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wasioona Mkoa wa Dodoma (TLB), Omary Lubuva, alisema bado kuna upungufu kwa baadhi ya wazazi na walezi kutoona umuhimu wa kuwapeleka shuleni watoto wenye ulemavu.

“Kama Serikali itaamua kuwasaka watoto hao kwa kushirikiana na jamii, tatizo hilo la kuwaficha majumbani litapungua,” alisema Lubuva.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles