|Veronica Romwald, Dar es salaam
Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) itaanza kuwafanyiwa upasuaji wa kupandikiza matiti kwa wanawake waliopoteza matiti kutokana na ugonjwa wa saratani.
Upasuaji huo kwa kitaalamu ujulikanao kama ‘Breast reconstruction after mastectomy’ utafanyywa kwa kurudishia tena kiungo hicho.
Mkurugenzi wa ORCI, Dk. Julius Mwaiselage amesema hospitali hiyo iko katika maandalizi ya kufikia hatua hiyo ya upasuaji wa kibingwa ikiwa ni moja kati ya makubaliano ya ushirikiano na Taasisi ya Saratani ya nchini China (Chinese Academy of Medical Science – Cancer Hospital).
“Saratani ya matiti ni miongoni mwa saratani zinaozoongoza kuwa na idadi kubwa ya wagonjwa wanaowapokewa na kuhudumiwa hospitalini hapa.
“Hivyo, tutashirikiana na wataalamu wenzetu kutoka katika Taasisi hiyo, upande wa upasuaji wa saratani hii, ikigundulika mapema si lazima kutoa titi lote, tunaweza kutoa ule uvimbe uliopo pale na kuacha titi lakini lazima uwe na mashine za kisasa za kutoa tiba mionzi (LINAC) ambazo tayari tunazo,” amesema.