25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

NYUMBA YA MWALIMU KITETO YAGEUZWA DARASA

Na MOHAMED HAMAD-MANYARA

NYUMBA ya mwalimu wa Shule ya Msingi Indorokoni, Kata ya Njoro wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara, imegeuzwa na kuwa darasa.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Diwani wa Viti Maalumu, Rehema Cheleleo (CCM), alipokuwa akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake.

Alisema kwamba, nyumba hiyo imegeuzwa na kuwa darasa baada ya baadhi ya wafugaji kutoona umuhimu wa elimu na kushindwa kujenga madarasa.

Kwa mujibu wa diwani huyo, shule hiyo ilifunguliwa mwaka 2011 kwa lengo la kuondoa kero ya wanafunzi wa jamii ya kifugaji kutembea umbali mrefu kwenda shuleni.

“Pamoja na jitihada za Serikali za kuboresha elimu, bado baadhi ya wazazi hawaoni haja ya  kusomesha watoto wao na hivyo kutoona umuhimu wa kujenga madarasa kwa ajili ya wanafunzi wao.

“Kwa hiyo, naiomba Serikali ifanye kila inaloweza ili ijenge madarasa shuleni hapa na kutokomeza kabisa tatizo hilo,” alisema diwani huyo.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Rashidi Itungi, alikiri kuwapo kwa tatizo hilo na kusema shule yake ina vyumba vitatu vya madarasa na nyumba moja ya mwalimu inayotumika kama darasa.

Pia, alisema inakabiliwa na uhaba wa vyoo pamoja na uchache wa walimu ambao hawatoshi kutokana na wanafunzi 400 walioko shuleni hapo.

Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Indorokoni, Sindilo Itemi, alisema baadhi ya wazazi wilayani Kiteto, wako tayari kuchangia sherehe kuliko wanavyofanya katika elimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles