24.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Nuno awawashia Wolves taa ya kijani

LONDON, ENGLAND

KOCHA wa timu ya Wolves, Nuno Santo, ameweka wazi kuwa anausubiri uongozi wa timu hiyo kumuwekea ofa mezani kwa ajili ya mkataba mpya.

Kocha huyo mkataba wake unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu wa 2021, lakini hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote ambayo yameanza kufanyika.

Msimu uliopita kocha huyo aliisaidia timu hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Europa kwa kushinda ubingwa wa Sky Bet Championship, ikiwa ni msimu wake wa kwanza. Katika msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita ilimaliza nafasi ya saba.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya FC Porto, aliongeza mkataba wa mwaka mmoja majira ya kiangazi mwaka jana, huku wenzake Dean Smith wa Aston Villa, Brendan Rodgers wa Leicester, Chris Wilder wa Sheffield United wameongeza mikataba mipya kipindi hiki, lakini Nuno bado.

“Uongozi haujafanya lolote hadi sasa na mimi sijawaambia lolote, lakini ukweli ni kwamba nimebakisha mkataba wa mwaka mmoja, hivyo siwezi kuwaza kwa sasa.

“Nilisaini mkataba msimu uliopita wa mwaka mmoja, hivyo kwa sasa nimebakisha mkataba wa mwaka mmoja, hivyo naweza kusema ukisaini mkataba unatakiwa kuutumikia kwa kipindi hicho mambo mengine ninaamini yanafuata baadae.

“Nina furaha na aina ya wachezaji nilionao hapa jinsi wanavyofanya kazi, kila kitu kinakwenda sawa, tunapambana ili kuhakikisha tunamaliza nafasi za juu, lakini nadhani huu sio muda sahihi ya kuzungumzia mkataba mpya, lakini wakati ukifika hakuna tatizo tutakaa chini na uongozi kwa ajili ya kujadili hilo,” alisema kocha huyo.

Jana Wolves ilikuwa kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao Leicester City kwenye mchezo wa Ligi Kuu nchini England, hivyo klabu ya mchezo huo Wolves ilikuwa inashika nafasi ya tisa ikiwa na pointi 35, wakati huo Leicester City wakishika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 49.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles