24.9 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Ndugai aonya mawaziri, wabunge watoro

Mwandishi wetu – Dodoma

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, amewataka wabunge na mawaziri kuhudhuria vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma bila kukosa na kwamba hiki ni kikao cha lala salama cha Bunge.

Akizugumza wakati Serikali ikiwasilisha Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na ukomo wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2020/21 mbele ya wabunge jijini Dodoma jana, Ndugai alionya kwamba hili ni Bunge la lala salama.

 “Ningewaomba sana mawaziri rekebisheni ratiba zenu kwa sababu hili ndio Bunge letu la lala salama, tunaomba sana pakitokea udhuru tutaambiana, kila waziri apatikane kwenye kamati na kwenye Bunge litakapoanza.

“Kamati zizingatie ratiba na wajumbe wote niwaombe muhudhurie na mzingatie muda ili kuliwezesha Bunge kutekeleza kwa usahihi. Kamati ziwe zinaweka kumbukumbu kwa ajili ya kuwasilisha.

“Natoa rai kwa Serikali nyaraka zote ziwasilishwe kwa wakati na waheshimiwa na mawaziri wahudhurie kwa wakati vikao hivyo kwa mujibu wa ratiba,” alisema Spika Ndugai.

Bunge linatarajiwa kuvunjwa na Rais Dk. John Magufuli mara baada ya kumalizika kwa Bunge la bajeti linalotarajiwa kuanza mapema Aprili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles