29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Nchi za ukanda wa A. Mashariki na Kati (CECAFA) bado zinajikongoja Afcon 2019

Lulu Ringo, Dar es salaam



Uganda ndio timu pekee kutoka nchi za Afrika ya Mashariki na kati (CECAFA) iliyofuzu kushiriki mashindano ya Kombe la Afrika (AFCON) mwakani yatakayofanyika nchini Cameroon mwakani.

Cecafa yenye jumla ya wanachama 12, kati ya hao Uganda pekee imefuzu ikiwa na alama 13 katika kundi L lenye timu ya Tanzania, Lesotho na Cape Verde.

Uganda imeshinda michezo minne, sare moja ilipocheza na Tanzania na sasa imebakisha mechi moja ya marudiano itakayopigwa Tanzania mchezo mmoja usio na madhara kwa Uganda.

Katika kundi L, timu tatu zilizobakia kila mmoja anahitaji kushinda mchezo uliosalia ili kufuzu kushiriki AFCON.

Uganda anaongoza kundi akifuatiwa na Lesotho mwenye alama 5 sawa na Tanzania wakipishana katika idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa huku Cape Verde akishika mkia kwa kuwa na alama 4. Michezo inayofuata Tanzania atakua nyumbani kumenyana na Uganda huku Cape Verde akimkaribisha Lesotho na kila mmoja kati yao akisaka alama 3 kwa hali na mali ili aweze kufuzu.

Timu zilizofuzu kushiriki AFCON hadi sasa ni Cameroon, Madagascar, Senegal, Mali, Algeria, Nigeria, Nigeria, Morocco, Ivory Cost, Mauritinia, Tunisia, Egypt, Tunisia na Uganda ambayo ni mwanachama wa CECAFA.

Timu wanachana wa CECAFA ni Burundi, Djibout, Eritrea, Kenya, Ethiopia, Tanzania, Uganda, Rwanda, South Sudan, Sudan, Somali na Zanzibar kati ya hao Uganda tayari ametangulia Cameroon na kitendawili kimebaki kwa Tanzania, Lesotho na Cape Verde.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles