25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

NCBA yaapa kusaidia ukuaji wa biashara za viwanda vidogo, kati nchini

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya NCBA imejipanga kusaidia biashara za viwanda vidogo na vya kati ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi.

Mkurugenzi Mkuu na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NCBA, Margaret Karume amesema hayo jana jijini Dar es Salaam katika kusheherekea uzinduzi wa benki hiyo nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Karume amesema malengo ya benki hiyo ni kuhamasisha wanaojituma kwenye safari yao ya mafanikio na kuchochea ukuaji wa kiuchumi nchini.

“Kupitia uvumbuzi wetu unaomzingatia mteja na uwekezaji kwenye bidhaa za kidijitali za benki, tuko tayari kuharakisha ukuaji na maendeleo katika sekta muhimu za kiuchumi kama vile biashara za viwanda vidogo, vya kati, mashirika, miradi mikubwa ya miundombinu na sekta ya kilimo.

“Nasisitiza kuwa juhudi zetu zitakuwa za kidijitali, Benki ya NCBA itawaweka watu na wateja wetu katikati ya uvumbuzi. Tutatendelea kuvumbua na kutoa huduma za bora za Kifedha na zenye viwango vya teknolojia ya juu zinazokubalika kimataifa na za kimapinduzi kama vile M-PAWA na huduma zingine za benki mtandao (online banking) ili kukidhi na kuvuka mahitaji ya wateja wetu,” amesema.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mipango, Dk. Ashatu Kijaji amesema Serikali inajitahidi kujenga uchumi wa viwanda juhudi ambazo zimejidhihirisha baada ya Tanzania kujumuishwa katika nchi yenye kipato cha kati kabla ya muda husika.

“Nathubutu kusema kuwa sekta ya kibenki ni nguzo muhimu katika kusaidia utoaji wa mali za Kifedha na upatikanaji wa mikopo kwa viwanda vidogo na vya kati.

“Mikopo hii mara nyingi huwa inawekezwa katika uendeshaji wa biashara, upanuzi, faida na kuongeza thamani kwa kila aliyeshiriki katika upatikanaji wa mapato na hili linaenda sambamba na maono ya Serikali.

Pamoja na mambo mengine, amesema ili tuwe na sekta imara ya Kifedha itakayoendesha uchumi jumuishi wa Kifedha nchini kote na kutoa bidhaa na huduma muhimu zitakazoongeza ukuaji wa kiuchumi wakati Sekta ya Kilimo inaendelea kuwa muhimu sana katia uchumi wetu kwa sababu inaajiri asilimia 70 ya watu nchini ambayo ina athari chanya katika ukuaji wa biashara za viwanda vidogo, vya kati na vyama vya ushirika.

“Hivyo basi, ukuaji katika sekta hii kupitia upatikanaji wa mikopo yenye riba nafuu, pembejeo, mafunzo ya kuwajengea uwezo na programu nyingine zitakazoongeza ufahamu wa Kifedha kwa wakulima na wafanyabiashara ni muhimu sana,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles