28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Nape atoa wito kwa kampuni za Tehama

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital 

Waziri  wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezitaka kampuni zinazoshughulika na Tehama, kuongeza  thamani za huduma wanazozitoa hasa katika afya ili kuwafikia wananchi wa kipato cha chini.

Amezungumza hayo leo Desemba 8, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na uongozi wa kampuni ya bima ya Jubilee, Airtel na Axieva kuhusu huduma mpya ya bima  ya gharama nafuu inayotarajiwa kuhudumia watu zaidi ya milioni 17.5.

Amesema serikali ya awamu ya sita imewekeza  katika miundombinu ya vituo vya afya na kuhakikisha inakuwa na vifaa vya kisasa ili kurahisisha huduma ya afya kwa wananchi wa kipato cha chini.

“Ili kuhakikisha kila mtanzania wa kipato cha chini ananufaika na  maendeleo yanayofanywa na serikali, kila mmoja aone namna  ya kutumia teknolojia. Natamani  kuona  jinsi Tehama  ikitumika  kuokoa maisha ya watu na itakavyobadilisha maisha yao hususani katika huduma za afya,” amesema Nape.

Amesema  serikali ipo tayari kumuunga mkono mtu yeyote atakayetumia teknolojia kuokoa maisha ya watu wanyonge.

Amesema watu wengi wakiwekeza  kwenye afya kupitia teknolojia  watasaidia kutoa mchango kwa Wizara ya Afya  na kuokoa fedha nyingi za matibabu  ndio maana hata serikali  imelenga  kwa kila Mtanzania  kupata bima ya afya kwa gharama nafuu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa  Jubilee, Dk. Harold  Andamson amesema  bima hiyo itakuwa ya gharama nafuu na kila mtanzania ataweza kuitumia  mara tu atakapolipa kupitia Airtel Money.

Pia amesema bima hiyo itatumika kwa zaidi ya vituo 642 ambavyo ni vya serikali lengo likiwa kuwafikia watu wenye kipato cha chini kuweza kunufaika na bima hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Airtel Money, Andrew Rugamba amesema ushirikiano wa kampuni hizo tatu ni mkakati  uliolenga kuleta mapinduzi  katika mazingira ya bima ya afya kwa  kutoa huduma nafuu zinazoendana na soko ambazo upatikanaji wake ni rahisi kwa watanzania  wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles