26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

NANHR kuja na mkakati wa kuwabana watendaji wa Serikali kufuata Katiba

Brighiter Masaki,Dar es Salaam

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Afrika (NANHRI), imeanzisha mkakati utakao wafanya watendaji mbalimbali wa taasisi za kiserikali kuanza kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia misingi ya sheria na katiba ili kukuza ustawi wa haki za binadamu.

Mpango huo unatekelezwa kwa kupitia azimio la mkataba wa Marrakech uliopitishwa na Umoja wa Afrika(AU) Mwaka 2018 ambapo taasisi za serikali zinapaswa kufanya kazi kwa kushirikina na haki za binadamu lakini pia wanatakiwa kulinda haki zao.

Akizungumza Dar es Salaam mapema Agosti 3, 2021 katika mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na tume hiyo kuwajengea uwezo watendaji wa taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Ofisi ya Mwendesha Mshtaka wa Serikali (DPP).

Mtendaji Mkuu wa (NANHRI), Gilbert Sebihongo amesema nchi nyingi za Afrika katika kutekeleza majukumu yao zinafanana na kumekuwa na malalamiko mengi lakini wanaamini kupitia mafunzo hayo watazingatia haki.

“Unajua hata hapa Tanzania kuna malalamiko mengi kwa wananchi namna serikali inavyokusanya kodi na vitu vingine na watendaji wanatakiwa kuwasikiliza na kuhakikisha wanatoa elimu ili nao waelewe kwakuwa ni wajibu wao kulipa kodi,”amesema Sebihongo

Sebihongo amesema kitendo cha kufanya mambo pasipo kuwasikiliza wananchi bado inakuwa sio haki na walianzisha mafunzo hayo kuwalenga watendaji hasa wale ambao shughuli zao zinagusa maisha ya wananchi muda wote.

Kwa upande wake Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, amesema mdau mkubwa wa kulinda haki za binadamu ni serikali hivyo watendaji wake wanapaswa kutekeleza hilo kwa vitendo.

“Kila mtu akisimama kwenye eneo lake kwa kuzingatia sheria ataweza kuwa mtetezi wa haki za binadamu kwa kufuata taratibu za kisheria bila kumuonea mtu kama upo mahakama kuacha vutendo vya kumbambikia watu,”amesema Olengurumwa

Naye Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, (THBUB), Mohamed Hamis Hamad alisema haki za binadamu ni suala mtambuka linahitaji mashirikiano kutoka kwa wote waten dawakifahamu hawa kama watetezi wa haki za binadamu watatumia nafasi zao kuingia kwenye mipango ya serikali.

“Haki za binadamu sio fasheni ni suala ambalo ni stahiki ya msingi ambapo kila binadamu anahitaji haki za kuishi ambazo toka anazaliwa anakuwa nazo na hizi sheria zingine zimekuja kusimamia tu.,”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles