27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MWIGULU AHAIDI KUMALIZA UJENZI WA ZAHANATI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Iramba magharibi mkoa wa Singida (kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa diwani wa kata ya Kinampanda Justus Makala kuhusu hatua za ujenzi wa zahanti ya kata ya Kinampanda jana.
Na Mwandishi Wetu, Singida

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM) ameahidi kumalizia mifuko 200 ya saruji na nondo 100 ili kukamilisha ujenzi wa Zahanati ya Kata ya Kinampanda.

Ahadi hiyo aliitoa mjini hapa jana baada ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo unaofadhiliwa na ofisi yake jimboni humo kwa kushirikiana na wananchi wanaochangia ujenzi huo.

“Kwa hatua ambayo mmeshafika hatuko mbali sana, wiki ijayo nitashuhulikia tupate saruji na nondo na nitaongea na mkandarasi na vijana wengine wapenda maendeleo wawepo hapa ndani ya wiki mbili wawe wameshafika juu na tunapomaliza mwaka wa fedha tuwe tushakamilisha ujenzi,” alisema.

Naye Diwani wa Kata ya Kinampanda (CCM),  Justus Makala, alisema kwa sasa kinachohitajika kwa haraka katika ujenzi huo ni saruji na nondo ili wapeleke jengo juu huku na aliwaomba wananchi wanajitolea kwa hali na mali kumsaidia Mwigulu kukamilisha zahanati hiyo.

Mmoja ya wananchi Mathayo Kahaya aliyefika eneo hilo alimshukuru Mwigulu kusaidia ujenzi wa zahanati hiyo huku akisema wananchi wana mwitikio mkubwa zaidi ya wa kuchangia ili ukamalike mapema.

Mwigulu jimboni humo kwa ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayofadhiliwa na ofisi ya mbunge akishirikiana na wananchi wa jimbo lake.

Miradi inayoendelea kwa sasa ni ujenzi wa hosteli 22 za wasichana katika kata zote na zahanati na visima vya maji zaidi 75 vya kisasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles