Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu operesheni maalum.
Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.
Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.
Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.
Kwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF) Luteni Kanali, Rais Museveni amempandisha afisa mkuu wa majeshi aliyeongoza operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa Rwenzururu, magharibi mwa nchi hiyo