32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto azaliwa kwa vinasaba vya watu watatu

dr-zhang-drupal

MEXICO CITY, MEXICO

WANASAYANSI wamethibitisha kuwa mtoto wa kwanza kabisa duniani amezaliwa kwa kutumia mbinu tata inayojumuisha vinasaba kutoka kwa watu watatu tofauti katika kiinitete.

Mtoto huyo mvulana alizaliwa nchini Mexico miezi mitano iliyopita na wazazi kutoka Jordan.

Anaripotiwa kuwa katika hali nzuri kiafya, kwa mujibu wa ripoti maalumu iliyochapishwa kwenye jarida la New Scientist.

Dk. John Zhang wa New Hope Fertility Centre mjini New York na timu yake walifanya utaratibu huo nchini Mexico ambako hakuna sheria inayozuia njia hiyo ambayo haijapitishwa Marekani.

Madaktari wa Marekani walichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa mtoto huyo wa kiume anakuwa huru dhidi ya kurithi jeni zenye kasoro za mama yake.

Wataalamu wanasema kuwa hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyingine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida, ambazo watoto huzirithi.

Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa Mitochondrial unahitajika.

Mitochondria ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini.

Baadhi ya wanawake hubeba jeni zilizo na kasoro na wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles