Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) umekuwa kivutio kwa wakazi wa Zanzibar kwa kuomba kupiga picha na bango la mradi huo wakati walipotembelea banda la Shirika la Umeme (Tanesco) katika maonesho ya Kimataifa ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Fumba.
Maonesho hayo yaliyoanza 7 Januari 7, 2024 ni jitihada za Serikali katika uwekezaji wa Sekta ya nishati nchini.
Mmoja wa wadau waliotembelea banda hilo ni Naibu Katibu Mkuu wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari, Selestine Kakele ambae ameonekana kuvutiwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ikiwamo mradi JNHPP ambao umefikia asilimia 95.83.
Naye Mwangulumba kutola Bodi ya Taifa ya Pamba, amesema kuwa mradi wa JNHPP ni tumaini jipya kwa Tanzania na kuwa utekelezaji wake umekua wa kipekee.
“Najiuliza tumewezaje kulifanya hili, huu mradi wa kipekee , maono ya waasisi wetu yalikua makubwa sasa hata wale wanatuoshangaa, hili tumeliweza,” amesema.
Kwa upande wake Issa Waziri mkazi wa Pemba, amesema kuwa mradi huo si kwamba utawapatia umeme wa kutosha lakini umekuwa kivutio kwa namna unavyoonekana.