28.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

MPANGO MKAKATI KUSAIDIA MIFUMO WIZARA YA AFYA WAZINDULIWA DAR

Na KASANDRA HASSAN (TUDARCO)

DAR ES SALAAM

TAASISI inayosaidia Wizara za Afya, Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya virusi vya Ukimwi na matibabu kwa kuimarisha mifumo ya afya ijulikanayo kama Tanzania Health Promotion Support (THPS) imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.

Akizindua mpango mkakati huo Dar es Salaam jana,  Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dk. Augustine Massawe alisema mpango huo ni wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 na 2020.

Alisema mkakati huo unalenga kusaidia juhudi za Wizara ya Afya, Serikali za mitaa na wadau wengine kutoa huduma bora za afya kwa magonjwa ya kuambukizwa na yasiyoambukizwa katika jamii.

Dk Massawe alisema anatarajia mpango huo utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS kwa kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri.

“Tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuhakikisha ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/Ukimwi.

“Nina matumaini mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na raslimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na  kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanyakazi kwa malengo”alisema Dk Massawe.

Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dk Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo kuwa ni pamoja na kuachana na VVU/ Ukimwi na kushughulika na magonjwa mengine tishio katika jamii,  kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.

Mradi huo unafadhiliwa Watu wa Marekani kupitia PEPFAR/ CDC na taasisi ya taifa ya afya Marekani (NHI), UNAIDS, Chuo Kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha Colombia na taasisi ya mfuko wa uwekezaji kwa watoto uliopoUingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles