Theresia Gasper -Dar es salaam
YANGA imeshindwa kutamba katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa jana, kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, baada ya kulamizishwa sare ya mabao 3-3 na Polisi Tanzania
Matokeo hayo ni kama Molinga ameiokoa Yanga kupata kichapo kutoka kwa Polisi Tanzania iliyotangulia kwa kufunga mabao 3-1 kabla ya mshambuliaji huyo kutupia mawili.
Katika mchezo wa jana, mabao ya Yanga yalifungwa na Mrisho Ngassa na David Molinga aliyefunga mawili huku Ditram Nchimbi akiifungia ‘hat-trick’ timu yake ya Polisi Tanzania.
Mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi, Abdallah Mwinyimkuu, Yanga ilikuwa ya kwanza kuandika bao dakika ya sita kupitia kwa Ngassa aliyemalizia kazi nzuri ya Juma Abdul.
Polisi Tanzania walifanya shambulizi nzuri dakika ya 22 baada ya Andrew Chamungu kupiga shuti na kupaisha.
Dakika ya 23 mchezaji wa Polisi Tanzania, Yassin Mustapha, alionyeshwa kadi njano kabla ya kupewa nyekundu kutokana na utovu wa nidhumu.
Naye kipa wa Yanga, Metacha Mnata alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 29 kutokana na kudaka mpira nje kidogo ya 18.
Polisi Tanzania iliweza kusawazisha dakika 33 kupitia kwa Nchimbi akimalizia mpira wa kona uliyochongwa nana Mustapha
Hata hivyo, Polisi Tanzania almanusura wapate bao la pili dakika ya 40, baada ya Marcel Kaheza kuipaisha shuti lake akiwa eneo la hatari.
Yanga walifanya shambulizi dakika ya 45, lakini mshambuliaji wa timu hiyo, David Molinga, alishindwa kufunga baada ya kupaisha shuti lake.
Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa zimefunga bao 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa Polisi Tanzania kulisambulia lango la Yanga na kuweza kupata bao dakika ya 55 lililofungwa na Nchimbi tena, akimalizia pasi ya mwisho ya Sixtus Sabilo.
Dakika dakika mbili baadaye, Ditram alifunga bao la tatu baada ya kuunganisha mpira wavuni kutokana na krosi Mustapha.
Molinga alifunga bao la pili kwa Yanga dakika 64 kwa kichwa kutokana na shuti la mpira wa adhabu uliopigwa na Abdul
Alikuwa Molinga kwa mara nyingine iliyeisawazishia Yanga dakika ya 68 kwa shuti la moja kwa moja la mpira wa adhabu.
Yanga; Metacha Mnata, Juma Abdul, Ali Mtoni, Kelvin Yondani, Lamine Moro, Abdulazizi Makame, Mrisho Ngassa, Feisal Salum, David Molinga, Juma Balinya/Mapinduzi Balama (dk 46) na Sadney Urikhob/ Deus Kaseke (dk 46).
Polisi Tanzania; Kulwa Manzi, William Lucian, Yassin Mustapha, Pato Ngonyani, Iddy Mobby, Baraka Majogoro, Andrew Chamungu, Hassan Maulid, Ditram Nchimbi, Marcel Kapama na Sixtus Sabilo/Mohammed Mkopi(dk70).