26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mlinga aitaka serikali kuhamasisha matumizi ya kondomu kwa uzazi wa mpango


Bethsheba Wambura

Mbunge wa Ulanga, Goodlucky Mlinga (CCM), amesema ongezeko la watoto wa mitaani nchini linasababishwa na watu kuacha kutumia mipira ya kike na kiume (kondomu) kama njia ya uzazi wa mpango.

Akiuliza swali bungeni jijini Dodoma leo Jumanne Juni 25, Mlinga alitaka kujua namna serikali inavyohamasisha watu kutumia mipira hiyo ili kuondokana na utitiri wa watoto wa mitaani.

“Mheshimiwa Spika, inafahamika wazi kuwa njia sahihi ya uzazi wa mpango ni kutumia mipira ya kike na ya kiume, suala la watu kutotumia mipira ya kiume licha ya watengenezaji kuweka vionjo mbalimbali katika mipira hiyo, je serikali ina mkakati gani wa kuhamasisha matumizi ya mipira hiyo?” amehoji Mlinga.


Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile amesema moja ya sababu ya watoto wa mitaani ni wazazi kutojiandaa kupata watoto na watu kupata ujauzito katika umri mdogo na kushindwa kuwalea.


“Kama serikali tumekuwa tukisisitiza njia za uzazi wa mpango likiwamo hilo la mpira. Suala hapa ni kujipanga katika malezi siyo kuzaa tu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles