Mkutano wa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, leo Alhamisi, Machi 23, 2017, umeahirishwa lakini pamoja na mambo mengine amelazimika kuongea na waandishi wa habari nje ya Ukumbi wa Hoteli ya Protea ili kuwafahamisha alichotaka kukisema.
Akizungumza na waandishi hao huku akiwa juu ya gari lake, Nape aliwaomba wamuunge mkono Rais akidai kuwa ndio Mungu amewapatia, na kuwa waitulize nchi kwakuwa hakuna sababu ya kuvurugana.
"Ninaombeni mumuunge mkono Rais wetu ndio tuliepewa na Mungu, tuitulize nchi hatuna sababu ya kuvurugana. Nape ni mdogo sana", alisema Nape
Huku akiwa na jazba baada ya kunyooshewa bastola na mtu wa usalama akitakiwa kutotoka nje ya gari, aliongeza kuwa, “Lengo la kuja hapa ni kumshukuru rais na mliotumwa hapa naomba mkafikishie. Nimefurahi sana kufanya kazi na nyie. Nawaombeni mmuunge mkono waziri mpya mliye naye", Nnauye
Hata hivyo, alisema kuwa hana kinyongo na rais kumtoa katika nafasi hiyo na kuwaomba wanahabri wampe ushirikiano Waziri Harrison Mwakyembe ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo.
“Kwasasa narudi jimboni Mtama kwa ajili yakuwatumikia wananchi. Nimekuwa mzalendo kwa nchi yangu na nimekuwa muungwana kwa nchi yangu na nitaendelea kuwa hivyo,” Nnauye
Awali, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kumteua waziri mpya wa habari na michezo.
Dkt Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambapo Nape Moses Nnauye ndiye aliyekuwa anashikilia wadhifa huo.
[embedyt] https://www.youtube.com/watch?v=oEdovxg2Fn0[/embedyt]