26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mjue Donald Trump, mshindi wa urais Marekani

donald-trump

Donald Trump ndiye Rais mpya wa Marekani baada ya kumshinda mpinzani wake Hillary Clinton kwa kupata kura za wajumbe 278, huku Clinton akiwa na 218. Mshindi alihitajika kupata kura 270 za wajumbe.

Donald Trump ambaye ataapishwa tarehe 20 Januari mwaka 2017, alizaliwa Juni 14 mwaka wa 1946, mjini New York, akiwa mtoto wa tano kati ya watoto sita.

Mama yake Donald aliyetambulika kwa jina la Mary ni mzaliwa wa Scotland lakini baba yake pamoja na babu yake walikuwa wahamiji kutoka Ujerumani na walikuwa wamiliki wa majumba makubwa ya kifahari.

Donald alisoma shule ya msingi mjini New York, baadae (1968) Chuo Kikuu cha Pennsylvania, akisomea elimu ya biashara.

Akiwa mjini New York, alifanya kazi katika kampuni ya babake ambaye aliendesha biashara ya kuuza nyumba kwa raia wa kipato cha wastani.

Ukizungumzia utajiri wa Trump ambaye ni mwanachama wa Republican, kwa tawkimu za Juni 2015, ana utajiri unaokadiriwa kufika  dola bilioni 8.7.

Lakini pia kuna tofauti kuhusu utajiri huo kwani Trump aliwahi kuiambia tume ya uchaguzi kwamba anao utajiri wa dola bilioni 10. Hata hivyo jarida la Forbes limenadi kwamba utajiri wa Trump haufikii juu ya dola bilioni 4.5.

Trump ambaye anakuwa ni Rais wa 45 kuiongoza Marekani sasa, aliwekeza katika biashara kubwa ya ujenzi na kuweza kujenga mojawapo ya mijengo ya kifahari zaidi nchini Marekani. Alifanikiwa kutokana na sera ya kiuchumi iliyokuwepo hasa ile ya mwaka 1980.

Mali alizofanikiwa kumiliki ni sawa na hoteli kubwa kubwa, viwanja vya mchezo wa gofu, makazi ya kifahari, majumba ya kamari kutoka Carlifonia hadi Mumbai huku nembo yake ikiwa ni Trump.

trump_

Vile vile, ameandika Riwaya kadhaa kuhusu biashara, huku umaarufu wake uking’aa zaidi katika makala yanayoelezea maisha halisi, “The Apprentice,” katika runinga ya NBC. Hata hivyo alitupwa nje ya makala hayo baada ya kutoa kauli zilizowakera raia wa Mexico.

Lakini pamoja na hili amekuwa mara kadhaa akishindwa katika biashara hizo na hadi kufikia kufungwa ama kufilisika hasa kipindi cha 1991 na 2009.

Kwa upande mwingine, ndoa za Trump zote tatu zimevunjika. Aliwahi kuwa mwanachama wa Democratic, na pia akajiunga na upande wa kujitegemea.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles