26 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Miss Tanga kujulikana Mei 6

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

FAINALI la shindano la kumtafuta mrimbwende wa Miss Tanga linatarajiwa kufanyika Mei 6, 2023 ambapo usahili wa warembo utafanyika Machi 18, mwaka huu katika ukumbi wa Tanga Resort.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Alhamisi Machi 16, 2023 jijini Dar es Salaam Mratibu wa shindano hilo, Victoria Martine, ambaye pia ni mbunifu wa mavazi amesema shindano hilo litakuwa na utofauti na mengine yaliyotangulia kutokana na uzoefu aliokuwa nao katika upande wa tasnia hiyo.

“Nimeshatwaa taji la miss Tanga mwaka 2007 nafahamu sheria na kanuni za shindano la urembo, hivyo nitahakikisha warembo kutoka nyumbani Tanga wanatimiza ndoto zao kupitia ulimbwende,” amesema Victoria.

Victoria ameongeza kuwa baada ya kukamilika kwa usahili kwa warembo wataingia kambini, Machi 29, mwaka huu kujifunza mambo mbalimbali ya urembo.

“Wito wetu kwa wadhamini kutusaidia ili kutimiza ndoto za wadogo zetu katika sekta ya urembo, pia kupeperusha vema bendera ya Taifa katika mashindano ya Kimataifa,” amesema Victoria.

Amesema kipindi warembo watakuwa kambini watapata nafasi ya kutembelea vivutio vilivyopo mkoani Tanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles