Aveline Kitomary, Dar es Salaam
Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali inatarajia kuanzisha mfumo wa kanzidata wa taifa utakaosaidia kurahisisha utambuzi wa miili iliyoharibika na watu wanaojihusisha na uhalifu kwa haraka zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es salaam wakati ya kuelezea mafanikio ya taasisi hiyo kwa miaka minne ya Rais Dk. John Magufuli amesema kazi data hiyo pia itasaidia katika matibabu.
“Tunatarajia kumaliza database hiyo ndani ya miaka miwili na tutahakikisha watu wote nchi nzima wataingia kwenye mfumo huo tutashirikiana na taasisi zingine.
“Database hii itasaidia kutambua miili iliyoharibika bila usumbufu wa kupima ndugu na pia kwa upande wa uhalifu kama mauaji, ubakaji ni rahisi kumtambua mhalifu bila kuchukua muda mrefu,” amesema Dk. Mafumiko.