32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mfanyabiashara ajishindia gari la kifahari droo ya Bonge la Mpango

Na Mwandishi Wetu, Sengerema

Abdallah Mohamed Abdallah, Mfanyabiashara, mkazi wa Morogoro ameshida zawadi ya gari mpya ya kisasa aina ya Toyota Fortuner katika droo kubwa ya kampeni ya Bonge la Mpango lililokuwa linaendeshwa na Benki ya NMB.

 Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Baraka Ladislaus akibonyeza kitufe ili kumpata mshindi wa promosheni ya Bonge la Mpango mkazi wa Morogoro Abdallah Mohamed Abdallah aliyejishindia Toyota Fortuner, baada ya droo ya mwisho kuchezeshwa Sengerema mkoani Mwanza,kushoto ni Msimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania Elibariki Sengasenga, Afisa Huduma kwa Wateja NMB Neema Deus(wa tatu kushoto) na Meneja wa NMB Sengerema Stanley Betty wakishuhudia.

Abdallah alijishindia gari hiyo ya kifahari yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 169 katika droo iliyochezeshwa mjini Sengerema mkoani Mwanza kuhitimisha kampeni ya Bonge la Mpango iliyoendeshwa kote nchini kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita.

Akizungumza wakati wakati wa droo hiyo iliyosimamiwa na Ofisa kutoka Bodi ya Taifa ya Michezo ya Kubahatisha, Elibariki Sengasenga, meneja wa NMB Kanda ya Ziwa, Ladislaus Baraka alisema ushindi wa Abdallah umekamilisha orodha ya washindi 148 waliojishindia zawadi mbalimbali zenye thamani ya zaidi ya Sh550 milioni tangu droo hiyo ilipozinduliwa mwezi Februari, 2021.

“Kupitia kampeni hii, benki ya NMB tumetoa zawadi ya fedha taslimu kwa washindi 120, pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya LIFAN 24, magari matatu ya mizigo aina ya Tata Ace maarufu kama kirikuu na gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner,” alisema Baraka

Alisema pamoja na kurejesha sehemu ya faida kwa jamii, kampeni ya bonge la mpango pia iliyolenga kuhimiza jamii kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba benki kwa ajili ya usalama badala ya kuhifadhi fedha majumbani.

Benki ya NMB imetenga zaidi ya Sh bilioni 1 kuchagia miradi ya maendeleo ya jamii katika sekta ya afya, elimu na misaada wakati wa majanga kwa mwaka huu wa fedha.

Akizungumza baada ya kujishindia gari, Abdallah aliishukuru benki ya NMB kwa zawadi hiyo huku akiwahimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha zao benki.

“Bado sijaamini kama kweli nimeshinda zawadi ya gari kwa sababu hata sikujua kama kuna droo inachezeshwa leo; sina mengi zaidi ya kuishukuru NMB kwa zawadi hii,” alisema Abdallah aliyenusurika kukosa zawadi kwa kuwa msikitini wakati alipopigiwa simu.

Kabla ya droo kubwa kuchezeshwa, mjasiriamali Faustine Nyawigrika, mjasiriamali anayemiliki duka la bidhaa za nyumbani mkazi wa Sengerema alikabidhiwa zawadi ya pikipiki ya mizigo ya miguu mitatu aina ya Lifan yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 4.5 aliyoshinda katika kampeni ya bonge la mpango.

Akizungumza wakati wa hafla ya kumkabidhi zawadi mshindi huyo, Meneja wa Benki ya NMB tawi la Sengerema, Stanley Betty aliwaomba wajasiriamali wakiwemo wafanyabiashara ndogodnogo, wakulima, wavuvi na wafugaji kujenga utamaduni wa kuhifadhi fedha benki kwa ajili ya usalama na kuongeza fursa ya kukopeshwa mitaji kuendeleza shughuli zao.

“Benki ya NMB tunatoa mikopo hadi kwa waendesha bodaboda kwa sharti la wakopoaji kuunda kikundi, kufungua akaonti na kuiendesha kwa kuweka na kutoa fedha kwa kipindi cha miezi mitatu kuwezesha maofisa wetu kufuatilia mwenendo wao wa mapato na matumizi,” alisema Betty.

Pamoja na huduma za kifedha, Betty alisema benki hiyo pia inatoa huduma ya bima za aina zote ikiwemo ya mali, mazao ya kilimo, mifugo na maisha huku akiwahimiza Watanzania kujenga utamaduni wa kukata bima ili kupata fidia wanapooata majanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles