27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

MEYA AWAONYA MAWAKALA MAEGESHO YA MAGARI

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.

Na CHRISTINA GAULUHANGA-DAR ES SALAAM

MEYA wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, amewataka mawakala wanaosimamia maegesho kuacha kuwabughudhi wamiliki wa magari kwa kuwakamata ovyo kwani kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, alisema ni vyema mawakala wakazingatia sheria ndogo za jiji na kuacha tabia ya kuwaonea wananchi wanaomiliki magari na kuyaegesha katikati ya jiji.

“Kuna tabia ya baadhi ya wafanyakazi kwenye makampuni ya uwakala ambao wamekuwa wakiwakamata kwa kuwaonea wananchi jambo ambalo si zuri, ni vyema wakazingatia mikataba kati yao na jiji,” alisema Mwita.

Alisema zipo kanuni ambazo jiji lilijiwekea, ambazo wakala anazifahamu, hivyo kukiuka ni kinyume na mkataba na atakayebainika atafutiwa uwakala.

Mwita alisema wakala anatakiwa kutoa muda wa dakika 60 kabla ya kuchukua uamuzi wa kuvuta gari, bodaboda au bajaji iliyovunja sheria.

“Lakini kwa gari, bodaboda au bajaji iliyozuia barabara itaondolewa mara moja ili kuondoa msongamano,” alisema Mwita.

Alisema wakala anaruhusiwa kuruhusu gari, pikipiki au bajaji kuegeshwa kwa dharura sehemu isiyoruhusiwa, kwa muda usiozidi dakika thelathini kama dereva ameweka viashiria vya tahadhari.

“Kama kuna dereva kapata dharura na imedhihirika hivyo, anaruhusiwa kuegesha gari yake hata dakika 60, tabia ya kukaa pembeni mawakala wanavizia mtu kaenda kununua vocha wanavamia gari yake hatutaki kabisa,” alisema Mwita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles