Na Imani Nathaniel, Tanga
Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa niaba ya Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri za Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2021, limetangaza kuongezwa kwa kundi moja la kushindaniwa na kufanya makundiwa kuwa 19 kwa sasa.
Akizungumza jijini Tanga leo Jumanne Desemba 14, 2021 Afisa Program wa MCT, Paul Malimbo, amesema kuongezwa kwa kundi hilo kunafuatiwa na ombi la Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzani (TCDC) ya kutaka kuwa na kundi ambalo litahusisha habari za vyama vya ushirika nchini ikiwa pamoja na shughuli za vyama vya Ushirika
Ikumbukwe kuwa tuzo hizi zilizinduliwa na Waziri Mkuu msataafu Joseph Warioba wakati wa kilele cha tuzo za 2020, Septemba 10,2021 zilizofanyika jijini Dar es Salam.
“Makundi mengine yanayoshindaniwa katika tuzo hizo ni tuzo ya Uandiahi wa habari za uchumi, Biashara na, tuzo za uandishi wa habari za michezo na utamaduni, tuzo za uandishi wa habari za elimu, tuzo za uandishi wa habari za kilimo na biashara, tuzo za habari za utalii na uhifadhi, tuzo za uandishi wa habari za uchunguzi na tuzo za uandishi wa habari za Data.
“Pia kuna tuzo za uandishi wa habari za haki za binadamu na utawala bora, mpiga picha wa bora, wapiga picha za gazeti na televisheni, mchora katuni bora, tuzo za uandishi wa jinsia na watoto, tuzo za uandishi wa habari za gesi na uchimbaji wa mafuta na madini, tuzo za uandishi wa habari za walemavu, tuzo za uandishi wa habari za afya, tuzo za uandishi wa habari za sayansi na teknlojia, tuzo za uandishi wa habari za hedhi salama, tuzo za uandishi wa habari za ushirika na kundi la wazi,” amesema.
Kwa upande wa Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoani Tanga, Henjewele John amewaomba waandishi wa habari kujitokeza kuandika habari za ushirika ili kuutangazia umma