30.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mchungaji aeleza kauli ya mwisho iliyotolewa na Mwandishi Mbonea

Tunu Nassor na Christina Gauluhuanga, Dar es salaam

MWILI wa Mwandishi wa Habari Eliya Mbonea, umeagwa jana Hospitali ya Taifa Muhimbili na unatarajiwa kuzikwa leo jijini Arusha huku mtu wa mwisho kuwa naye wodini akieleza kauli yake ya mwisho kabla ya kukata roho.

Mbonea hadi anafikwa na umauti alikuwa akiandikia magazeti ya Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, akiwa mwakilishi wake kwenye mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Mchungaji wa Kanisa la Anglikana, Joseph Opio jana alisema wameshindwa kufanya ibada ya kuaga mwili wa marehemu kwa sababu Serikali imezuia ibada hizo kwa sababu zinakutanisha watu wengi wakati huu wa janga la corona.

Akizungumza na MTANZANIA, Mchungaji Opio alisema amepatwa na mshtuko kutokana na kifo cha Mbonea.

Alisema siku ya kifo chake alikuwa naye wodini ambapo alikuwa akijiandaa kupata ruhusa ya kutoka na muda mfupi akaletewa matunda akaomba aingie chooni kwanza.

Alisema cha kushangaza baada ya kutoka chooni akasema anajisikia vibaya kwakuwa ametapika alivyoingia chooni.

“Tulishangaa kwa dakika chache akajilaza kitandani na kuanza kulalamika anaishiwa hewa na wakaja madaktari wakajaribu kumwongezea oksijeni, lakini ikashindikana na ndio ikawa mwisho wa Mbonea.

“Inauma sana, baada ya hali hiyo alimwita kaka yake na kumwambia ‘ninakufa naomba nisaidie kunitunzia mke wangu na watoto pia’, akakata roho,” alisema Mchungaji Opio.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles