Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro
Wananchi wa Kijiji cha Kilomeni wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro wamejitolea nguvu kazi kubeba mawe kwa ajili kujenga vyumba vya madarasa ya shule ya msingi Mlevo ambalo imetakiwa kubolewa ili kupisha ujenzi wa barabara .
Wakizungumza katika tamasha la Msaragambo ambalo limeandaliwa na diwani wa Kata Kilomeni nakumshirikisha Mbunge wa Jimbo Mwanga, Joseph Tadayo, wamewema shule hiyo imejengwa tangu mwaka 1975.
Dorah Mvungi amesema wananchi wataendelea kushirikiana kujitolea nguvu kazi mpaka Shule itakapokamilika.
Diwani Kata Kilomeni, Mhamed Mgala amesema kuwa mkakati ya kuanza kujenga shule mpya ni kutokana na majengo shule zamani ya Shule mlefo kutakiwa kubolewa Tanroad kitokana na kwamba yapo kwenye miundombinu za barabara ili kupisha ujenzi wa barabara.
Amesema madarasa hayo matatu yatachukua siku tisini hadi kukamilika ili wanafunzi wahamishwe kwenye majengo mapya na kuweza kuendelea na masomo.
“Barabara inatakiwa mita 30 kulia na miata 30 kushoto hivyo shule hii ilitakiwa kubomolewa kwani ipo ndani ya miundombinu ya barabara na Tanrod wanataka kujenga barabara, naomba niwahakikishie wananchi kwamba ndani ya siku tisini tutakuwa tumemaliza ujenzi wa madarasa matatu,” amesema.
Mbunge wa Mwanga, Joseph Tadayo, amewapoengeza wananchi kujitolea nguvu kwa ajili ya shughuli za Maendeleo nakuahidi kuendela kushirikiana kwa hali na mali kukamilisha ujenzi huo.
Mbunge huyo pia amechangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ujenzi vyumba vitatu vya madarasa.