25.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Ilemela anuwia kuibua vipaji vya soka

Na Sheila Katikula, Mwanza

NAIBU Waziri wa Aridhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela mkoani Mwanza, Dk. Angelina Mabula ameeleza kiu yake ya kuibua vipaji vya soka mkoani Mwanza kupitia mashindano ya Angelina Cup.

Dk.Mabula amesema hayo katika hitimisho la mchezo wa fainali wa mashindano hayo yaliyohusisha takribani michezo 42 kwa timu tofauti jimboni humo kuchuana kushindania kombe hilo.

Amesema mchezo wa soka ni miongoni mwa fursa wanazoweza kutumia vijana kukabiliana na changamoto ya ajira hivo mashindano hayo yataendelea kuwepo ili kuwapa nafasi vijana kuonyesha kile walichonacho katika soka.

“Kwa hiyo mashindano haya tuneyaanzisha kwa malengo makuu matatu, kwanza ni kuibua vipaji vya vijana katika jimbo la Ilemela, la pili ni kuhakikisha wanapata ajira kutokana,” amesema.

Naye mgeni wa heshima katika mchezo wa fainali katika mashindano hayo, Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama Cha Mapinduzi kutoka mkoa wa Mwanza, Jamal Babu amesema jitihada za kuandaa mashindano hayo ni za kipongezwa.

Babu amesema mashindano ya michezo ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya CCM ambapo mashindano hayo yameweza kuwakutanisha vijana kwa kuwa michezo imekuwa sehemu ya uchumi wa taifa na ndio maana Rais Samia Suluhu amewekeza katika michezo.

“Kama mlivyosikia Rais Samia ametoa takribani Shilingi bilioni 9.5 kwa ajili ya kuhakikisha vile viwanja ambavyo viko wazi vinawekwa miundombinu rafiki kwa ajili ya michezo, lakini ametoa bilioni 1.3 kuendeleza timu za taifa ikiwemo zile za wanawake,” amesema Babu.

Katika mashindano hayo ya Angelina Cup timu ya soka ya kata ya Kirumba iliibuka bingwa wa mashindano hayo kwa kuifunga timu ya kata ya Ibungilo kwa penati 4 kwa 3 baada ya timu hizo kutoka sare 1-1 ndani ya dakika 90 za mchezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles