27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

MAUWASA kujenga tanki la kuhifadhi maji Maswa

Na Samwel Mwanga,Maswa

Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA) iliyoko katika wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeanza ujenzi wa tanki lenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni moja kwa siku.

Mkurugenzi Mtendaji wa MAUWASA, Mhandisi Nandi Mathias, amesema ujenzi wa tanki hilo ni mpango wa muda wa uboreshaji wa huduma ya maji safi na salama mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa chujio la maji katika chanzo kikuu cha maji katika bwawa la New Sola lililoko kwenye kijiji cha Zanzui.

Akiongea katika eneo ambalo tanki hilo litajengwa katika kilima cha Nyalikungu mjini Maswa amesema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo pia kutasaidia kupunguza gharama za uendeshaji.

“Tumekuwa tukisukuma maji kwa wananchi kwa masaa 11 kwa sasa kuanzia saa 10.00 alfajili hadi saa 8.00 mchana kwa siku ila tanki likikamilika  tutasukuma maki kwa masaa mawili tu,”amesema.

Amesema kuwa ujenzi wa tanki hilo utagharimu kiasi cha fedha Sh milioni 497 na tayari serikali imeshatoa kiasi cha Sh milioni 100 na jtafanyika kwa kutumia mfumo wa Force Account.

Amesema kwa sasa shughuli hizo za ujenzi zimeshaanza  katika eneo hilo na shughuli za awali zitakuwa ni ujenzi wa kitako na ujenzi wa ukuta.

Amesema kuwa ujenzi huo unategemea kutoa ajira za muda kwa zaidi ya wananchi 250 katika mji wa Maswa kwa maelekezo ya serikali ya awamu ya sita ya kutaka miradi yote inayojengwa kwa Force Akaunti iwashirikishe wananchi walio wengi wa eneo husika.

Aidha katika hatua nyingine,Mhandisi Nandi ametoa wito kwa wananchi kuitunza na kuilinda miundo mbinu ya maji inayojengwa na serikali na kuwafichua watu wote watakaohujumu miundo mbinu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles