29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Marekani yaishitaki kampuni ya Huawei

WASHINGTON, MAREKANI

SERIKALI ya Marekani imeifungulia mashitaka kampuni kubwa ya teknoplojia ya China, Huawei,  kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha, kuzuia utekelezaji wa haki na wizi wa teknolojia.

Kesi hiyo huenda ikazua mgogoro wa biashara kati ya Marekani na China hali ambayo pia itaathiri biashara ya kampuni hiyo inayokuwa kwa kasi duniani.

Katika taarifa, Huawei imesema  imekasirishwa  na mashtaka dhidi ya yake.

Imesema   haikufanya makosa yote yanayodaiwa ilitekeleza na kwamba haina ufahamu wa kosa alilofanya binti wa mwasisi wa kampuni hiyo, Meng.

Meng alikamatwa  Canada mwezi uliyopita kufuatia ombi la Marekani, kwa madai ya kukiuka vikwazo vyake dhidi ya Iran.

“Kwa miaka kadhaa sasa, kampuni za China zimekiuka sheria zetu za biashara ya  mataifa, hatua ambayo inahujumu vikwazo vyetu na mara nyingine kutumia mfumo wa fedha wa Marakani kuendesha shughuli zao haramu. Hili lazima likomeshwe,” alisema Waziri wa Biashara wa Marekani, Wilbur Ross.

Wizara hiyo inadai Huawei iliipotosha Marekani na Benki ya Kimataifa na kufanya biashara na Iran kupitia kampuni zake mbili za mawasiliano, Huawei Device USA na Skycom Tech.

Utawala wa Rais Donald Trump ulirejesha vikwazo vyote dhidi ya Iran vilivyokuwa vimeondolewa chini ya mkataba wa kimataifa wa nyuklia uliofikiwa mwaka 2015.

Kesi ya pili inadai kuwa Huawei iliiba teknolojia kutoka Kampuni ya T Mobile kufanyia majaribio ya kudumu pamoja na kupinga sheria na ubadhirifu wa fedha kupitia mtandao.

Huawei ni moja ya kampuni kubwa za mawasiliano na usambazaji wa simu duniani, ambayo hivi karibuni iliishinda Apple na kuwa ya pili kwa uundaji wa simu aina ya smartphone baada ya Samsung.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles