WASHINGTON, MAREKANI
SERIKALI ya Marekani na China zimeonyesha hali ya kujipa matumaini ya kumaliza mvutano wao wa kibiashara ambao ulisababisha kuwekeana vikwazo.
Kauli hiyo ya matumaini ya kumaliza mvutano wao imetolewa na mjumbe wa Rais wa Marekani, Donald Trump, katika mazungumzo ya kibiashara na China, Robert Lightizer, ambaye amesema hayo baada ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa China, Liu He.
“Makubaliano muhimu ya kibiashara yatafikiwa. Maendeleo yameweza kupatikana wakati wa mazungumzo yao,” alisema Robert Lightizer.
Kwa upande wake, Rais Xi Jinping wa China ameandika katika risala yake anatarajia pande hizo mbili zitaendelea kushirikiana katika hali ya kuheshimiana. Pindi makubaliano yakishindwa kuafikiwa hadi Machi mosi inayokuja, Rais Trump anapanga kuzitoza ushuru wa asilimia kati ya 10 na 25 bidhaa zote zitakazoingia Marekani kutoka China.