32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AAGIZA MAENEO YA MAGEREZA YAPIMWE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amemwagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa kusimamia upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na magereza nchini kote na kuhakikisha yanawekewa mipaka.

Ametoa agizo hilo jana, wakati wa kikao kati ya  Kamishna Dk. Malewa na maofisa magereza wa mikoa yote na maofisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma.

“Magereza yetu mengi yako maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na magereza. Lazima tuyapime na kuyawekea alama mipakani,” alisema.

Mbali ya maeneo hayo,Majaliwa alisema jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo yamechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi.

“Natambua jeshi hili lina mashamba makubwa nayo pia hayajapimwa. Kila Mkuu wa Magereza wa Mkoa (RPO), ni mjumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapima ardhi kutoka kwenye halmashauri zenu,mhakikishe maeneo hayo yanapatiwa hati,”alisema.

Alisema umefika wakati sasa kila gereza litambue na kuainisha fursa walizonazo ili waweze kuamua ni kwa kiasi gani wanaweza kujitegemea kwa uzalishaji. “Kama ni kilimo, ufugaji, au uzalishaji wa umeme, tuangalie ni kipi kinaweza kuvutia uwekezaji,  cha msingi zaidi ni lazima tuwe na hati za maeneo tuliyonayo,” amesema.

Alisema kuna baadhi ya magereza yalikuwa maarufu kwa kilimo, lakini hivi sasa hakuna hata moja lenye trekta na kama yapo ni moja au mawili tu.

Kuhusu ufugaji na uvuvi wa samaki, aliagiza jeshi hilo litumie maofisa wake waliobobea kwenye sekta hizo, watumike kuendeleza na kuhamisha ujuzi wao kwa wafungwa wanaotumikia vifungo ili wanapotoka gerezani, wawe na ujuzi.

Amesema ili kukabiliana

Kwa upande wake, Dk. Malewa alisema atafuatilia suala la upimaji wa maeneo ya magereza kwa sababu wanao wapimaji na vifaa wanavyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles