33.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 22, 2024

Contact us: [email protected]

Machinga Dar kuondolewa mitaani

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

JOHANES RESPICHIUS, DAR ES SALAAM

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ametoa siku 14 kwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuhakikisha wanawaondoa wamachinga katika maeneo yasiyo rasmi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makonda alisema uamuzi huo umekuja baada ya Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Dar es Salaam kupoteza mapato ya zaidi ya Sh bilioni 100 kutokana na wafanyabiashara wakubwa ambao si waaminifu kukwepa kodi kwa mtindo wa kuwapa bidhaa wamachinga ili kuuza barabarani.

Alitolea mfano wa Manispaa ya Ilala peke yake, Makonda alisema ndani ya mwezi mmoja uliopita imepoteza Sh bilioni 54.

“Sasa wamachinga wameanza kutumika na watu wenye mizigo waliyohifadhi kwenye magodauni ambapo wamekuwa wakienda kuchukua mizigo na kuanza kuuza mitaani kwa bei wanazozitaka baadae anarejesha kiwango walichoahidiana…namna hii ya kupoteza mapato hatuwezi kujenga uchumi wa nchi yetu.

“Ninachoomba wamachinga wale ambao wana maeneo yao warudi walikokuwa na ambao walikuwa hawana sehemu zimeshaandaliwa, hivyo basi wawaone wakuu wao wa wilaya kwenye wilaya zao watawapangia maeneo stahiki.

“Wakuu wa wilaya nimewapa siku 14 kuhakikisha kila machinga anakaa sehemu stahiki, kuna sehemu za masoko zimebaki na ushuru haikusanywi watu wamekimbilia barabarani,” alisema Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles