26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Maambukizi ya virusi vya corona yazidi kupanda, maofisa China watimuliwa

Beijing, China

VIFO vya watu  242 vilivyotokana na virusi vya corona vimerekodiwa kwa siku Jumatano tu  katika jimbo la Hubei, ikielezwa kuwa ni idadi kubwa kuwahi kutokea

Pia kulikuwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya watu 14,840 waliogundulika kuwa na virusi hivyo.

Kutokana na hilo, China imewafukuza kazi maofisa wake wawili wa juu katika jimbo la Hubei saa kadhaa baada ya idadi  mpya ya walioambukizwa virusi hivyo  kutangazwa.

Maambukizi mapya na vifo katika eneo hilo imefanya idadi ya vifo kufikia 1,350 na maambukizi ya watu karibu 60,000.

China imekuwa ikishutumiwa kutoweka wazi uhalisia wa ukubwa wa tatizo hilo.

Profesa David Heymann, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza kutoka Chuo cha madawa jijini London amesema:

” Kilichotokea nchini China ni kuwa wamebadili mantiki kuhusu maana ya ugonjwa, sasa wanawachukua watu wenye viashiria vichache.

”Vifo vinatisha, kuna ongezeko la vifo limeripotiwa, lakini ukitazama kwa ujumla, idadi ya vifo na maambukizi bado ipo juu, kama vifo vinavyotokana na mafua.”

Kwa ujumla jimbo la Hubei lina maambukizi ya watu 48,206 yaliyothibitishwa.

Katika hatua nyingine, nafasi ya Katibu wa chama cha kikomunisti Hubei, Jiang Chaoliang, imechukuliwa na mkuu wa chama katika jimbo la Shanghai Ying Yong.

Kulingana na vyombo vya habari vya China, Mkuu wa chama katika mji mkuu Wuhan pia amevuliwa majukumu yake.

Ni mabadiliko ya kwanza makubwa kufanyika yakiwahusisha maofisa wa chama katika jimbo Hubei tangu kutokea kwa mlipuko huo

Mapema wiki hii, idadi kubwa ya maofisa wa afya waliondolewa kazini.

Jimbo la Hubei linachukua zaidi ya 80% ya maambukizi nchini China.

 Maambukizi hayo sasa yanajumuisha visa vilivyogunduliwa kliniki katika idadi ya visa vilivyothibitishwa.

Hii inamaanisha ni pamoja na zile zinazoonesha dalili, na kuwa na skani ya CT inayoonesha mapafu yaliyoathirika, badala ya kutegemea tu vipimo vya nucleic acid.

Kati ya vifo vipya 242 mjini Wuhan, 135 ni vile vilivyotambulika kwa vipimo vya kliniki.

Hii ina maanisha kuwa, hata bila njia mpya, idadi ya vifo Hubei siku ya Jumatano ilikuwa 107, ikiwa ni idadi kubwa kwa jimbo hilo.

Kwa ujumla jimbo la Hubei lina maambukizi ya watu 48,206 yaliyothibitishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles