29.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Ludewa yakabiliwa na uhaba wa walimu 400

Na Mwandishi Wetu, Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, Andrea Tsere, amesema wilaya hiyo inakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa walimu zaidi ya 400 na kuiomba Wizara ya Elimu kuangalia namna ya kuwaongezea ili kupandisha kiwango cha ufaulu wilayani humo.

Akizungumza katika kikao cha watumishi wa halmashauri ya Ludewa, Tsere amesema mfumo unaotumika kuajiri walimu sio rafiki kwa maeneo ya pembezoni.

‘’Tunaupungufu mkubwa wa walimu nawalimu wanaajiriwa na TAMISEMI ambayo iko Dodoma na kwa awamu zilizopita waliajiri walimu kwa kutumia kanuni ya idadi ya wanafunzi kwa walimu.

“Kanuni hii sisi huku tunaonewa tunaomba wabadili kanuni kwa shule zilizopo wilaya za pembezoni watumie kanuni ya mikondo kwa walimu, shule moja iwe na walau walimu saba tunaomba hilo,’’amesema Tsere.

Mbunge wa jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga, ameahidi kwenda kulitafutia ufumbuzi suala hilo huku akiwataka walimu waliopo kuwa wazalendo kwa kufanya kazi kwa bidii pamoja na kuendelea kushughulikia changamoto zilizopo ndani ya uwezo wao.

‘’Nitakwenda kufuatilia lakini niwaombe walimu kuwa wazalendo tufanye kazi kwa bidii ili tupandishe ufaulu katika wilaya yetu,changamoto tutazitatua kwa pamoja msisite kunishirikisha.

“Wakati umefika sasa watumishi kushirikiana kwa sababu tayari uchaguzi umeisha hivyo tutumie muda uliopo kufanya kazi ili kuongeza mapato ya halmashauri hii,” amesema Kamonga.

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ludewa, Bakari Mfaume amesema kila mtumishi anapaswa kufanya kazi kwa kutizama Ilani pamoja na kutokutumia nguvu katika kutatua kero za wananchi.

‘’Watumishi achaneni na maswala ya kisiasa kwa sababu uchaguzi umekwisha fanyeni kazi kwa kukubali viongozi walichaguliwa’’amesema Mfaume.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles