31.8 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

LUAGA MPINA AWEKA REHANI UWAZIRI WAKE

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ameweka rehani uwaziri wake akisema kuwa endapo   uvuvi haramu hautakoma ndani ya   mwaka mmoja atajiuzulu wadhifa wake.

Pia amesema kwa yeyote atakayebainika kuhusika kwa namna moja ama nyingine na biashara haramu ya uvuvi, atafilisiwa mali zake   na kupelekwa mahakamani.

Hayo aliyasema   Dar es Salaam jana  baada ya kutembelea  Kituo cha Uvuvi cha TAFICO  ambako alikagua vifaa vinavyoshikiliwa na kituo hicho kutoka kwa wavuvi haramu.

Alisema kazi ndiyo imeanza na atahakikisha katika   mwaka mmoja anapambana kufa na kupona kuhakikisha uvuvi haramu unakwisha, mapato serikali yanaongezeka  na kuwapo uwekezaji mkubwa katika sekta ya uvuvi.

“Hatuwezi kukosa mapato kupitia uharibifu unaofanywa na waroho wa fedha.

“Hatuwezi kukosa kitoweo, ni lazima suala hili lidhibitiwe iwe kwa kuwafilisi na kuwapeleka mahakamani wahusika wakuu na itakua fundisho kwa wengine wenye lengo la kufanya hivyo,”  alisema Mpina.

Alilihusisha suala la uvuvi haramu na magonjwa akisena kutokana na kukithiri kwake,    wananchi wanaokula samaki hao wapo hatarini kuugua kansa na matumbo ya kuhara.

Alisema kwa kuendelea uvuvi haramu taifa linapata hasara ya Sh bilioni tatu huku gharama halisi za fedha zinazotokana  na uvuvi zikiwa ni Sh trilioni mbili,   hali  inayotokana na wavuvi hao kukwepa kulipa kodi.

Alisema hakuna haja ya serikali kuhangaika na wavuvi haramu huku wasaliti wanaoshirikiana nao wakiwa ndani, hivyo ipo haja kuanza kuwasimamisha kazi watumishi hao na wengine wanaohisiwa kushirikiana nao.

Alimtaka  Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayesimamia uvuvi, Yohana Budeba, kutembea na barua za kuwasimamisha  kazi watumishi wanaokutwa na makosa ya kushirikiana na wavuvi haramu na aache sehemu ya kuweka jina ambalo litabandikwa papo hapo .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles