29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Lipumba aitaka serikali kufunga mipaka

Christina Gauluhanga na Sabina Wandiba – Dar es salaam

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameiomba serikali kuhakikisha inafunga mipaka haraka kuzuia wageni wanaoingia nchini ambao nchi zao zimekumbwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 19, Profesa Lipumba amesema kuendelea kuacha mipaka hiyo bila udhibiti wa wageni hao ni kuendelea kuhatarisha usalama wa afya za wananchi.

Amesema ni vema kukaongezwa uwezo wa vipimo na wataalamu wa kutosha ili kuwabaini wasafiri wanaoingia nchini wanaotoka sehemu mbalimbali za nchi.

“Wakati sasa umefika wa serikali kuamua kufanya uamuzi wa kufunga mipaka yetu, kuweka wataalam na vifaa vya kutosha kwani ugonjwa huu ni hatari na ukiendelea kuingia hapa nchini hali itakuwa mbaya zaidi kwakuwa hata mataifa tajiri wanahangaika nao,”amesema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba ameongeza kuwa wataalamu wasiishie kupima tu kiasi cha joto bali ni vizuri wakajiridhisha zaidi kwa kuchunguza ffya ya wasafiri hao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles