27.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

KUBENEA, GWAJIMA WAFUNGUKA KUHUSU LISSU

Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea (Chadema), amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anawakumbuka kwa sura watu waliompiga risasi.

Akizungumza katika Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es Salaam leo Septemba 10, Kubenea amesema kama Jeshi la Polisi litawakamata watu hao, Lissu anaweza kuwatambua kwa sura.

Aidha, amesema mmoja kati ya waliompiga risasi alikuwa amevaa kofia na miwani nyeusi na kwamba walianza  kumfuatilia kuanzia Tegeta jijini Dar ambapo baada ya kugundua anafuatiliwa kwa kuwa gari yake ni kubwa, aliweza kuwakimbia hadi Dodoma na kuwaacha.

“Lakini pia si kweli kwamba Tundu Lissu alipigwa risasi 28 hadi 32, bali alipigwa risasi 38, polisi waliokota maganda ya risasi 30 ya SMG na risasi nane za bastola, walipopiga risasi Lissu alilala mbele ya kiti cha dereva, lakini wauaji walijua kalaza kiti chake kwa nyuma hivyo wakapiga risasi 25 kiti cha nyuma.

Kwa upande wake mdogo wa Lissu ambaye naye alishiriki ibada hiyo ya kumwombea Lissu kanisani hapo, amewataka Watanzania kuendelea kumwombea kaka yake anayeendelea na matibabu katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya ambapo pia amemwelezea kuwa alikuwa mpenda haki tangu akiwa mdogo.

Naye Askofu Gwajima amelaani tukio hilo ambapo amesema katika somo lake la leo ni damu isiyo na hatia ambapo kupitia somo hilo alionya watu wanaomwaga damu za wenzao bila hatia kuwa nao damu zao zitamwagika vivyo hivyo.

Lissu alipigwa risasi  na wati wasiojulikana Alhamisi wiki hii, nyumbani kwake Area D, mkoani Dodoma wakati akitoka bungeni.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles