27.3 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

KIPO KITU ZAIDI YA KUAMBIWA UNAPENDWA…

NA JOSEPH SHALUWA

UNAWEZA kumkuta mtu anatabasamu peke yake, anajisikia amani baada ya kumaliza mazungumzo na mpenzi wake, kisha mwishoni wakamalizia na “I love you baby,” naye akamjibu: I love you too my sweet darling.”

Maneno ya mapenzi kama hayo huleta faraja sana kwenye uhusiano, lakini kwa bahati mbaya kuna wengine ni matajiri wa kutamka maneno ya namna hiyo, lakini mioyo yao inasoma kitu cha tofauti kabisa.

Usidanganyike kwa kuitwa majina mazuri. Muhimu ni penzi la dhati. Unatumia njia gani kumchunguza mwenzi wako kugundua kuwa ni kweli anakupenda kwa dhati na siyo kuishia kusema I love you pekee?

Hili ni somo muhimu sana kufahamu kwa wanandoa na ambao wanatarajia kuingia kwenye ndoa. Hebu tujiulize, unaposema; nakupenda, unamaanisha nini?

Tulia kwa muda, tafakari…mpenzi wako anapokuambia anakupenda, unafikiri nini zaidi kichwani mwako? Marafiki hapo ndipo kwenye msingi mzima wa mada yetu. Wengi huishia kufikiri kirahisirahisi tu, kuwa anampenda fulani au mwezi wake anampenda!

Je, umewahi kujiuliza, unampenda mpenzi wako kwa kiwango gani? Je, yeye anakupenda kwa kiasi gani? Upendo wake unamaanisha nini hasa? Upendo wako kwake una maana gani? Ni pendo la ndani kweli au tamaa za mwili?

Unaweza kujiuliza, inawezekana vipi, ukampenda mtu hadi mkafikia kuingia kwenye ndoa, bado ikawa ni tamaa ya ngono tu? Hapa namaanisha kuwa yawezekana vipi, mpendane halafu muingie ndani maelewano yaondoke?

Heshima itoweke? Upendo utoweke? Inawezakana vipi? Wengi wanajiuliza: “Tumependa na mume wangu kwa miaka mingi, tumeingia kwenye ndoa na tumeishi humo kwa siku nyingi lakini kwa nini leo hii nimuoene amebadilika?”

Wasomaji wengi wananiuliza maswali yanayofanana na hayo (hasa wanawake). Ngoja nikupe kisa cha msomaji mmoja mwanamke, kisha tuingie kwa undani zaidi katika mada yetu.

KUTOKA KWA MSOMAJI:

Mimi nipo kwenye ndoa kwa miaka sita sasa, mimi na mume wangu tumejaliwa kupata watoto wawili – wa kike na wa kiume. Miaka mitatu ya mwanzo tuliishi kwa amani na upendo, nilipojifungua mtoto wa pili ndipo mabadiliko yakaanza.

Nimejikuta sina msisimko kabisa na mume wangu. Yaani nikimwangalia namuona wa kawaida tu, hanishawishi kwa chochote. Tatizo ni nini? Naomba ushauri wako.

TUJIFUNZE KUTOKA KWAKE

Naamini wanawake wengi wana tatizo kama hilo. Si wanawake tu, hata wanaume nao wapo ambao hawana mvuto tena kwa wake zao. Wanaona wa kawaida kabisa, hakuna msisimko wala ushawishi.

Wanatazamana kama magogo tu, maana hakuna jambo jipya linaloonekana mbele ya uso wa macho yao. Ni kweli, tatizo hili lipo, tena linatafuna sana ndoa nyingi. Swali la msingi hapa, kama msomaji huyo anakiri alimpenda mumewe kwa dhati, wakafunga ndoa, iweje leo abadilike?

Ikiwa alikubali kwa hiyari yake kuunganishwa na mumewe, tena hadi wamefikia hatua wamezaa, mapenzi yamekwenda wapi? Hapo ndipo kwenye somo lenyewe ambalo bila shaka ndiyo itakuwa tiba ya wote wanaosumbuliwa na tatizo hili.

KUPENDA NA KUPENDWA

Kitu cha msingi ambacho unatakiwa kujifunza hapa ni kwamba, pendo la dhati huishi ndani. Penzi huwa haliishi, halina muda maalum wa kuishi ndani ya mtu. Kwa maneno mengine ni kwamba, kama ulimpenda miaka 20 iliyopita kwa dhati ya moyo wako, basi leo huwezi kumchukia.

Upendo ukishaingia ndani ya moyo wa mtu hubaki humo milele, ila kuna mambo madogomadogo au pengine yanaweza kuwa makubwa, yanayoweza kusababisha kuuhairisha upendo kwa muda.

Nasema kuuhairisha kwa sababu hauwezi kuondoka. Rafiki zangu, ujue wazi kuwa, hadi mwenzi wako ameamua kuungana na wewe katika ndoa, si bahati mbaya. Hajabahatisha, bali amekuchagua kutoka kwa wengi.

Kama ndivyo, kwa nini penzi liondoke ghafla? Haiwezekani. Kwa maana hiyo, sasa ni wazi kuwa, penzi huharibiwa na sisi wenyewe. Kuna mambo ambayo yakifanyika hupunguza nguvu ya mapenzi na mwisho wake kusababisha matatizo kama nilivyoeleza hapo juu.

Mada yetu itaendelea wiki ijayo, USIKOSE!

Je, unapenda kujifunza masomo haya zaidi kwa njia ya simu? Wasiliana nami kwa simu 0712 170745/0763 255818.

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Saikolojia ya Uhusiano. Ameandikia vitabu vingi vikiwemo True Love, Let’s Talk About Love na Maisha ya Ndoa. Kwa sasa anaandaa kitabu

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles