30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

KIMBUNGA MANGKHUT CHATIKISA CHINA

BEIJING, China


WAKAZI wa maeneo mbalimbali nchini hapa wamewekwa katika tahadhari, baada ya mvua kubwa zinazoambatana na upepo uliosababishwa na kimbunga kikali cha Mangkhut kuanza kuelekea maeneo ya Pwani ya Kusini mwa nchi hii.

Mpaka sasa watu zaidi ya 100 wanaripotiwa kujeruhiwa katika mji wa  Hong Kong, ambako kimbunga hicho kimeezua mapaa ya nyumba na kuvunja vioo vya madirisha na milango.

Kimbunga hicho pia kinaripotiwa kusababisha vifo vya watu 30 nchini Ufilipino, lakini maeneo ambayo kimesababisha madhara makubwa bado hajaripotiwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, mjini  Hong Kong, mamlaka za huko zimeweka hali ya tahadhari ya wastani kwa wakazi kukaa ndani ya nyumba zao ili kujihadhari na vitu vinavyopeperushwa na upepo huo ambao unakadiriwa kuwa na kasi ya kilomita 117 kwa saa.

Maofisa wa Serikali katika mji huo wanasema kuwa mpaka sasa  waliojeruhiwa ni watu 111, lakini mwandishi wa BBC, Robin Brant, aliyepo mjini humo anasema kwamba huenda madhara yaliyosababishwa na upepo huo yakawa ni makubwa zaidi.

Mwandishi huyo wa BBC anasema kwamba kiwango cha maji kimeongezeka na kufikia futi 12 na kwamba samaki ambao wapo hai wamekuwa wakisambaa mitaani.

Alisema maduka na huduma za kijamii zimefungwa na safari zaidi ya 800 za usafiri wa ndege zimeahirishwa  katika Uwanja wa Kimataifa wa mjini  Hong Kong na hivyo kuwaathiri abiria zaidi ya  100,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles