32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kihongosi aagiza Wenyeviti, Makatibu wa mikoa kuanzisha Klabu za Jogging

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Taifa  (UVCCM), Kenan Kihongosi amewaagiza Wenyeviti na Makatibu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uanzishwaji wa Klubu za Jogging katika maeneo yao lengo likiwa ni kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasio ya kuambukiza.

Akizungumza leo Julai 31, wakati wa uzinduzi wa Klabu ya ufanyaji mazoezi ya Vijana Jogging Mkoa wa Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri jijini hapa, Kihongosi ameagiza Makatibu na Wenyeviti wa CCM mikoa na wilaya kuanzisha klabu za Jogging za vijana katika maeneo yao.

Amesema utaratibu huo utasaidia vijana kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza pamoja na kuiweka miili vizuri.

Aidha, amefanya mazoezi kuanzia katika viwanja vya Nyerere Square hadi katika uwanja wa Jamhuri pamoja na vijana wa mikoa ya Arusha, Iringa na Dodoma wakiwamo wanafunzi wa Vyuo Vikuu, Shule za Sekondari na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde.

“Utaratibu wa Vijana Jogging Club itakuwa ni kwa nchi nzima, wenyeviti na makatibu wa mikoa na wilaya naagiza wafanye utaratibu katika mikoa na wilaya ili waanzishe hizi Club,”amesema Kihongosi.

Katibu Mkuu huyo pia amewataka vijana kujitokeza kupata chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19 ambayo ni ya hiari huku akisisitiza kuendelea kufanya mazoezi ili kujikinga na ugonjwa huo.

“Chanjo ni hiari tuhamasishe watu wapate chanjo uhai wa mtu ni yeye mwenyewe wale wenye fursa nendeni mkachanje akili za kuambiwa changanya na zako, kikubwa fanyeni mazoezi kujikinga na corona,”amesema.

Vilevile, Katibu Mkuu huyo amewataka watanzania kuendelea kuilinda amani iliyopo ambapo amesisitiza ataendelea kuwa mtumishi wa wote katika kuhakikisha vijana wanafikia malengo yao.

Kwa upande wake, Mbunge Mavunde amesema anafurahi kuona UVCCM ikihamasisha kuendelea kufanya mazoezi ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na umoja huo kuhakikisha wanafikia malengo.

“Nafurahi UVCCM mnashirikisha vijana ni vyema kuendelea, nikuahidi tutakuwa bega kwa bega kufikia malengo na matarajio,”amesema Mavunde.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dodoma, Bill Chidabwa amesema wataendelea kuwa mabalozi wa umoja huo kwa kuhakikisha wanafikia malengo yao waliyojiwekea ikiwa ni pamoja na kufanya mazoezi mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.

Nae, Diwani wa Kata ya Sekei Mkoani Arusha, Gerald Sebastian amesema vijana wa Dodoma wamepata bahati kuwa karibu na Kihongosi kwani ni mchapakazi huku akiwataka kushirikiana nae na wampe ushirikiano ili mambo yaende vizuri.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles