25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

KENYA: MWALIMU WA SAYANSI PETER TABICHI ASHINDA TUZO YA DUNIA

Na Mwandishi Wetu

Mwalimu wa sayansi nchini Kenya , ambaye hutoa sehemu kubwa ya mshahara wake kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi maskini zaidi, ameshinda tuzo ya dola milioni moja ($1m ) kwa kuwa mwalimu bora zaidi duniani kwa mwaka 2019.

Peter Tabichi, ambaye anatoka katika Shirika la kidini la Francisco, amesifiwa kwa mafanikio yake katika shule yenye madarasa yenye watoto wengi pamoja na vitabu vichache.

Akiwa kama mwalimu Peter amekuwa akitaka kuwaona watoto wa shule wakiichukulia sayansi kama njia ya kufuata  kwa ajili ya siku zao zijazo.

Tuzo hiyo ilitangazwa katika sherehe iliyofanyika mjini Dubai, ambapo alitambuliwa kama mwalimu aliyejitolea kufanya kazi isiyo za kawaida kwa watoto katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la bonde la ufa nchini Kenya.

Mwalimu Peter hutoa asilimia 80 ya mshahara wake kuwasaidia watoto katika Shule ya kutwa ya Sekondari ya wasichana na wavulana ya Keriko iliyopo katika kijiji cha Pwani, kaunti ya Nakuru, ambao hawana uwezo wa kupata sare za shule na pamoja na vitabu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles