26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Kanisa la Anglikana kuongeza idadi ya ibada kupambana na corona

Janeth Mushi, Arusha

Katika kukabiliana na kupambana na maambukizi ya virusi vya corona nchini, Kanisa la Anglikana Tanzania, limejipanga kupunguza msongamano wa waumini kwa kuongeza idadi ya ibada zake.


Hayo yamesemwa leo Alhamisi Machi 19, jijini Arusha na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikan Tanzania, Dk. Maimbo Mndolwa ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Tanga, baada ya kumalizika kwa kikao kilichoshirikisha maaskofu wake 28 kutoka Dayosisi zote zilizopo Tanzania Bara na Visiwani.


“Moja ya tahadhari tunazochukua ni pamoja na kupunguza idadi ya watu katika ibada kwa kuongeza ibada kama vile; mahali penye ibada moja sasa kutakuwa na ibada mbili,” amesema.


Kikao hicho mbali na ajenda hiyo kimejadili kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa hilo nchini tangu mwaka 1970 yanayotarajiwa kufanyika makao makuu ya kanisa hilo yaliyopo mkoani Dodoma Septemba mwaka huu.


“Kutokana na hali hiyo, tumeelekeza kila Dayosisi itenge siku maalumu ya maombi kuanzia leo Machi 19 na Ibada ya Ijumaa Kuu, itakuwa siku ya ibada ya pamoja ya Kanisa Anglikana Tanzania kuombea Taifa letu dhidi ya virusi hivyo vya corona,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles