Na Arodia Peter, Kigali
Rais Paul Kagame wa Rwanda na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), amefungua rasmi mkutano wa majadiliano kuelekea kutia saini makubaliano ya kulifanya Bara la Afrika kuwa na soko huru la biashara na uchumi wa pamoja.
Katika uzinduzi huo, Kagame alisema huu si wakati wa Afrika kuangalia ilikojikwaa, bali kuchukua hatua kwa vitendo ili kuwezesha waafrika kuamua uchumi wao kwa uhuru.
Aidha, Kagame amesema soko hilo litapunguza vikwazo baina ya nchi na nchi na hivyo kila mmoja kuthamini na kutumia bidhaa zinazozalishwa Afrika.