27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jose Chameleone apata pigo afiwa na mdogo wake AK47

Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI wa dancehall, Emmanuel Mayanja (AK47) ambaye ni mdogo wa mwanamuziki Jose Chameleone, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kudondoka vibaya akiwa bafuni.
Mayanja, ambaye ndiye mdogo pekee wa Chameleone aliyebaki katika lebo yake ya Leon Island Records, baada ya Weasel na Pallaso kujiengua, anaelezwa kufariki dunia katika mji wa Kabalagala, Kampala nchini Uganda,
Kifo chake kilithibitishwa na madaktari baada ya kufikishwa katika hospitali ya Nsambya iliyopo katika eneo hilo.

Baadhi ya taarifa katika mitandao mbalimbali nchini humo inaripoti kwamba mwanamuziki huyo alikumbwa na mauti hayo baada ya kutokea ugomvi katika moja ya baa zilizopo kitongoji cha Kabalagala.
Baada ya ugomvi huo aliumizwa usoni, hivyo akaamua kwenda bafuni kwa lengo la kufuta damu zilizokuwa zikimtoka, lakini akiwa huko alianguka akajigonga kichwani akapoteza fahamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles