30.4 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

JKT watamba kujipanga zaidi Nanenane mwaka huu

Na Derick Milton, Simiyu

Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania (JKT), Meja Jenerali Martin Busungu, amesema kuwa jeshi hilo limejipanga zaidi ya mwaka jana katika maonyesho ya Sikukuu ya Wakulima maarufu Nanenane kitaifa yatakayofanyika katika viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu.

Meja Jenerali Busungu amesema hayo leo Jumatatu Julai 29, wakati akiozungmza na waandishi wa habari kwenye viwanja hivyo, mara baada ya kukagua shughuli mbalimbali zilizoandaliwa na jeshi hilo zitazoonyeshwa kwenye sikukuu hizo.

Amesema mwaka jana jeshi hilo liliibuka mshindi wa jumla kwenye maonyesho hayo, ambapo ameeleza kuwa wameboresha zaidi katika nyanja za kilimo, ufugaji, ufundi na ujasiriamali na kuwataka wakulima kwenda katika eneo la jeshi hilo kwa ajili ya kujifunza zaidi.

“ Mwaka huu tumejiandaa kwa kiwango cha hali ya juu zaidi, wakulima wategemee kuja kuona jinsi JKT inavyoshiriki kwenye kilimo, ufugaji, mazao ya misitu, mazao ya wanyama, na nimeridhishwa na maandalizi yote,” amesema Meja Jenerali Busungu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Antony Mtaka ameendelea kuwakaribisha zaidi wananchi hasa wakulima, wafugaji na wajasliamali kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo kwa ajili ya kupata elimu, teknolojia na bidhaa mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles