29.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Jaye wa Cameroon awatamani Diamond, Vanessa Mdee, Victoria Kimani

NA CHRISTOPHER MSEKENA

WASANII wenye asili ya Afrika, wameendelea kupenya kwenye anga la Kimataifa huku lebo zinazomilikiwa na Waafrika wenzao zikisimamia mchongo mzima. Miongoni mwa lebo hizo ni BGC Melody yenye makao makuu yake California, Marekani.

BGC Melody ni lebo yenye asili ya Cameroon, imejikita katika kuinua na kukuza vipaji vya wasanii wa Afrika ndio maana licha ya kuwa na makazi yake Marekani, wana tawi dogo nchini Cameroon.

Mrembo Jaye ni mmoja ya wasanii wanaosimamiwa na BGC Melody na leo amefanya mahojiano mafupi na Swaggaz ili kujitambulisha kwa mashabiki wa Afrika Mashariki hasa Tanzania.

SWAGGAZ: Jaye ni nani?

Jaye: Jina langu ni Mbeng Julie Ike, kwenye muziki natumia Jaye, nilizaliwa miaka kadhaa iliyopita Kaskazini Magharibi mwa Cameroon kwenye Mji wa Muyuka ila nilikulia Kusini Magharibi kwenye miji ya Kumba na Limbe ambako huko nilianza shule.

SWAGGAZ: Ulianza lini kujishughulisha na sanaa ya muziki?

Jaye: Nilianza muziki nikiwa na miaka nane, hapo nilitambua nina kipaji na inatakiwa nikiindeleze. Mwaka 2013 niliachia wimbo wangu wa kwanza unaoitwa Sweet Mother uliotengenezwa na prodyuza Salatiel.

Lakini niliacha muziki na kurudi shule baada ya kumaliza masomo nimerudi kwenye muziki mwaka jana kwa kishindo cha nguvu kuliko ilivyokuwa hapo awali nikiwa hapa mjini Buea.SWAGGAZ: Ulipata vipi nafasi ya kusainiwa na lebo ya Marekani BGC Melody?

Jaye: Nadhani waliona kipaji changu kwa kutazama nyimbo nilizofanya hapo nyuma ndio maana wakavutiwa na mimi.

Nilisaini mkataba na BGC Melody hivi karibuni na nikafanikiwa kutoa ngoma kama Un Genre Une Genre (Afro Dance) ambayo ilitengenezwa na Sango Edi na mpaka sasa YouTube imetezamwa na watu 141,014, Amio yenye mahadhi ya Kizomba ikiwa imetengenezwa na Marc Ef mpaka sasa imetanzamwa na watu 410,153.

SWAGGAZ: Bila shaka unafuatilia muziki wa Afrika Mashariki, je ni wasanii gani unatamani kufanya nao kazi?

Jaye: Kwa sasa natazama mbele zaidi na ninataka kufanya kazi na wasanii wa Afrika Mashariki hasa Vanessa Mdee, Diamond Platinumz, Mwasiti and Victoria Kimani.

SWAGGAZ: Umewaandalia nini mashabiki zako wapya kutoka Tanzania?
Jaye: Jana nimeachia wimbo wangu mpya unaitwa Bad Energy, video ipo kwenye YouTube katika chaneli ya BGC Melody pia Septemba 18, mwaka huu nitatoa albamu mpya inayoitwa U Can’t Be Me itakuwa na nyimbo 18 kwahiyo mashabiki zangu wa Bongo naombeni sapoti tusizi kuusukuma muziki wa Afrika uende duniani.

Pia kwa mashabiki zangu wote tunaweza kuwasiliana WhasApp na manager wangu kupitia + 703 566 4404, + +237 679 240 030, [email protected] na kwenye mitandao ya kijamii Instagram napatikana kwa majina ya @queenjaye237 au kwa kugusa link ya https://youtu.be/Ibn1AVG-kL0 kutazama video zangu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles